Posts

Showing posts from May, 2018

Ufisadi hautoisha tanzania

Magufuli na uwanja wa ndege Chato Ansbert Ngurumo anaandika 6th May 2018 RAIS John Magufuli amekamatika. Sababu za yeye kutopenda kukosolewa, na bidii yake kudhibiti wapinzani hata kwa kumwaga damu, zimeanza kujulikana. Anaogopa wapinzani na vyombo vya habari wasiibue ufisadi wake au wa rafiki zake. Katika siku za hivi karibuni, mbali na “upotevu” wa Sh. 1.5 trilioni ambazo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) amesema hakuona zilipo, huku serikali ikijitahidi kufunika sakata hili kwa maelezo yasiyoeleweka, na bila mafanikio, kuna wizi mwingine wa kimfumo unaohusisha Rais Magufuli na watu wake wa karibu. Rais Magufuli anatajwa katika dili la Uwanja wa Ndege wa Chato, ambao ulipangiwa kujengwa kwa Sh. 39 bilioni, lakini hadi sasa umetumia Sh. 42 bilioni, ambazo zimepitishwa bila idhini ya bunge. Wanaojua kinachondelea wanasema fedha hizo nazo “zimepigwa.” Wanachosikitikia ni kwamba rais anajua na anahusika, hata kama mkono wake hauonekani moja kwa moja. Kampun