Posts

Showing posts from April, 2018

UNAZI WETU UNAUWA SOKA

Wachambuzi wengi na watangazaji wa mpira tumefeli sana kwenye tukio la kelvin kumtemea mate kwasi. Tukio limekuzwa mno limekuwa ndio story kuliko hata mechi yenyewe na hii nikutokana na baadhi ya wachambuzi wengi kuingia uwanjan wakiwa na matokeo Kelvin alifanya kazi kubwa kuhakikisha okwi na boko hawapi nafasi kabisa ya kuuchezea mpira aliziba njia zote wakishilikiana vizuri na dante  Wengi walitaraji yanga itafungwa gori nyingi na ndio wakwanza kupiga kelele na hii sio kuwa kweli kosa lile liliwakela hapana kilichowakela ni kushindwa kupata matarajio ya matokeo yao Ukiwasikiliza sana wanaolilia kwenye vyombo vya habali niwale wale ambao walitoa utabili wao kuwa simba itashinda kwa kishindo wakimaanisha kwa gori nyingi Hoja yao kubwa ni simba iko vizuri msimu huu imewasajili wachezaji wazuri kwa garama kubwa wakati yanga wachezaji wake sio wapambanaji hawako vizuri wakisahau kuwa mpira ni dak 90 na yeyote anaweza kushinda Nijuzi tu ambapo yanga ilikuwa inacheza na singida

Uozo wa mawaziri

    Source kwinyara Mawaziri wanakuja na pop up majibu kwa report ya CAG, yaani ndani ya wiki mbili sijui wanakua wameshafanya marekebisho. Alafu tunataka kuamini kweli wamerekebisha, report inayobeba madudu ya mwaka mmoja, leo gafla wawe wamesharekebisha na kucover minyoo yote walioiachia muda wote huo. Watanzania puuzeni hayo majibu ya hao Mawaziri njaa, maana report ya CAG mwaka ujao wa fedha wizara hizo hizo mtaona huo ubadhilifu kama kawaida ndio mtaamini hawana lolote hao wanajaribu kuziba ushuzi kwa kiwango cha kiganja. Hayo masifa wanayo mjaza JPM mara katoka kwa Mungu, mara wamuunge mkono, huku matrilioni yanapotea kwa mwaka yanapigwa juu kwa juu. Inaonyesha huu ulaji wa sasa ni wa watu wachache sana, kama wakina Bashite wakina Gambo, lazima wawe mabilionea wezi. Alafu ile mahakama ya mafisadi walishindwaga kuifungua kisa nini? Wanajijua wezi hao. CCM ni ile ile Watanzania tuandamane kuhakikisha hawa adui wa ustawi wa nchi yetu wanaondoka enzini. By onesmo