UNAZI WETU UNAUWA SOKA

Wachambuzi wengi na watangazaji wa mpira tumefeli sana kwenye tukio la kelvin kumtemea mate kwasi.

Tukio limekuzwa mno limekuwa ndio story kuliko hata mechi yenyewe na hii nikutokana na baadhi ya wachambuzi wengi kuingia uwanjan wakiwa na matokeo

Kelvin alifanya kazi kubwa kuhakikisha okwi na boko hawapi nafasi kabisa ya kuuchezea mpira aliziba njia zote wakishilikiana vizuri na dante

 Wengi walitaraji yanga itafungwa gori nyingi na ndio wakwanza kupiga kelele na hii sio kuwa kweli kosa lile liliwakela hapana kilichowakela ni kushindwa kupata matarajio ya matokeo yao

Ukiwasikiliza sana wanaolilia kwenye vyombo vya habali niwale wale ambao walitoa utabili wao kuwa simba itashinda kwa kishindo wakimaanisha kwa gori nyingi

Hoja yao kubwa ni simba iko vizuri msimu huu imewasajili wachezaji wazuri kwa garama kubwa wakati yanga wachezaji wake sio wapambanaji hawako vizuri wakisahau kuwa mpira ni dak 90 na yeyote anaweza kushinda

Nijuzi tu ambapo yanga ilikuwa inacheza na singida kelvin huohuo alifanyiwa tukio kama hilo hilo na kotinyo ambapo ilileta tahaluki na mpira ukasimama kwa dak moja mwamuzi alioneshwa mate yale sikioni wote tuliona lkn hakuna mchambuzi alosimama na kupiga kelele

 leo tukio hilo linafanywa na kelvin kila mtu ndo habari kubwa tumefukia kitendo alichokifanya kichuya kwa kesy na mwamuzi kafumbia macho

Tumemkalia kimya okwi ambae alifanya vitendo ambavyo sio vya kiungwana dhidi ya kipa youthe wakati anaanzisha mpira  alimsukuma kaanguka chini refa hakuona

Najiuliza hivi kosa kutema mate au mate ya kelvin kwenda kwa kwasi? Kosa hili limeanza leo au lipo kama lipo na mamlaka husika zipo

 tukio zililiona kwa nn tunazielekeza kazi ya kufanya kwamba ichukue hatua na wengine wanahoji kabisa sijui inakaa lini? Mbona hatoi hukumu mala apigwe faini , mwingine asimamishwe mechi nashindwa kuelewa kuwa ivi sheria zipo tunazifwata au matukio yakitokea ndipo tunatunga sheria

 Nakubali kumtemea mate mtu nitendo baya lkn isiwe ndio habali tunauua mpira tunauwa vipaji vya wachezaji wetu tusiwe na midomo michafu pindi wachezaji wetu wanapoteleza tuweke pembeni unazi tuuchambue mpira

By onesmo righton mwaki

Comments

Popular posts from this blog

NYOTA YA MZALIWA WA KWANZA

SANAA NI NINI?

STORY YA UTAKE