Siasa mchezo wa hovyo sana
SIASA BANA
Inafahamika wazi na wengi tumeaminishwa kuwa siasa ni mchezo mchafu
Kwa sasa hii iko wazi ukiangalia siasa zetu na viongozi wetu tanzania jinsi zinavyokwenda na jinsi mambo yanavyoendeshwa
Kama kuna kipindi ambacho vyama vya siasa vinatakiwa kuwa makini nikipindi hichi cha hama hama ya viongozi ambayo imekuwa ikisikika kila kukicha
Watu wamepokea kwa hisia tofauti hamahama hii, wapo wanaodai kuwa kuhama kwa viongozi ni kudhofisha chama flani na kuimalisha kingine
Wengine wanasema hii nijanja janja ya chama ili kujua mbinu ya mpinzani wako lazima ukae karibu nae na ikiwezekana ule nae kabisa kwa lengo la kumwaminisha kuwa upo upande wake
Kuna watu hawataki kabisa kuamini katika hayo yote wao wamejikita katika msimamo wa kuwa uoga na njaaa ndio chanzo cha wao kuweza kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine
Lakini ukirudi nyuma ukasikiliza tamko alilolitoa aliekuwa mwenyekiti wa vijana Bavicha patrobas katambi kuhusiana na tukio la mh tundu lissu ambae alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi akiwa kwake dodoma
Patrobas kupitia mkutano na wandishi wa habari 23 sep alisema kama polisi watashindwa kuwapata wanaowaita wasiojulikana tutawatafuta wasiojulikana kwa njia zisizo jilikana na tutukigundua kuwa asiejulikana ndie asie julikana tutamshugurikia kwa njia zisizo julikana
Lkn kiongozi huyo leo yuko chama cha mapinduzi ccm je tuamin kuwa hii ndio njia isiojulikana aloichukua katambi ya kuwatafuta wasiojulikana au ule mpango wake wa kuwatafuta ameuahirisha je ninjaa?
Maswali hayo msomaji waweza kujiuliza ukakosa majibu ya kueleweka zaidi zaidi utabaki kuvishauri vyama vya siasa kuwa viwe makini sana na watu wanaowapokea
Wengi hoja zao ni kuunga mkono jitihada ya dhati alonayo rais wetu john pombe magufuri wakati wengine wanasema wanataka kupigania demokrasia ya kwel.
Je tumuamini nani na nani tusimuamin wakati huo kumbuka tayari tumekalilishwa kuwa siasa ni mchezo mchafu
B
Comments
Post a Comment