ALIE PIGWA NA RADI MWAKA JANA AFARIKI DUNIA

Mtu mmoja mkaazi wa mloo mbozi mbeya amefariki usiku wa kuamkia leo kufuatia maumivu makali alokuwa akiyapata kwa kipindi cha mwaka mzima baada ya mwaka jana mwezi wa kumi kupigwa na radi akiwa kirabuni kunywa pombe ya kienyeji.

mtu huyo ambaye alifahamika kwajina la bambuji kalakana alipigwa na radi kirabuni hapo baada ya kutokea mzozo na mtu mmoja aliefahamika kwa jina moja la donard ambae inasadikiwa kuwa alikuwa akimdai sh 1500 baada ya kunywa pombe zenye thamani ya pesa hiyo .

akiongea na mwandishi wa habari hizi mmoja wa ndugu wa marehem kwa mashariti ya kutotajwa jina alisema ilikuwa jumapili ambapo yeye na ndugu yake marehemu walikwenda kilabuni kunywa pombe lakin marehemu hakupewa pombe alizoagiza ndipo mabishano yakaanza kumbe marehem aliwa anadaiwa kilabuni hapo.

anasema baada ya mda kidogo mvua zikaanza kunyesha ndipo radi ikapiga nakuchana suruari ya mbambuji na alikuwa akiyasikia maumivu makari huku akiomba msamaa akimtaka mdai wake amsamee wakati huyo donard alikuwa hayupo kirabuni hapo

pia alitanabaisha kuwa marehemu ameugua kwa mda wa mwaka mmoja sasa tangu amepata mkasa huo na kwamba walijaribu kuzunguka nae katika hospitari mbali mbali ikashindina ndipo wakamuua kumpeleka kwa waganga wa kinyenyeji ambapo kila walipo fika kwa waganga wa kienyeji walikuwa wakiambiwa ndugu yao ameshakufa tayari

hata hivyo wakazi wengi wa eneo hili wanahusisha tukio la kifo cha bwana bambuji na imani za kishikina kwa madai kuwa bwana donard amekuwa akifanya matukio kama haya kwa watu wengi ambapo kila mtu anae zozana nae au kumcheleweshea hela zake lazima akumbwe na maswaiba kama hayo

sanjari na hayo waliongeza kuwa kuna bwana mmoja ambae alikuwa mshindani wake kibiashara alimuunguzia ledio  yake kwa radi lakini alipoenda mwenyewe aliigusa kidigo kwa mkono ledio ikaanza kuimba kama kawada baada ya hapo akamtaka ahame kirabuni hapo vinginevyo angefanyia vitu vikubwa zaidi ya hilo  

Comments

Popular posts from this blog

NYOTA YA MZALIWA WA KWANZA

SANAA NI NINI?

STORY YA UTAKE